Habari

Baadhi ya washukiwa ujambazi nyumbani kwa Fina Mango wakamatwa, ni mtandao wa majambazi 40

Baadhi ya washukiwa ujambazi nyumbani kwa mtangazaji wa kipindi cha Makutano cha Magic FM, Fina Mango wamekamatwa.Kwa mujibu wa Fina, majambazi hao wapo kwenye mtandao mkubwa unaofanya vitendo hivyo jijini Dar es Salaam.

Fina Mambo akiwa na familia yake
Fina Mambo akiwa na familia yake

Kupitia Twitter ameeleza:

Lile kundi la majambazi lilokua likifanya uvamizi wa nyumba zipatazo 7 (kwangu ilikua ya 4) maeneo ya Kawe hadi Mbezi, ilisemekana ni kundi la watu 40 waliosambaa kuanzia Kawe (makao makuu) Mikocheni, Kinondoni mpaka Mbagala, Wameanza kukamatwa.

Polisi Kawe inashikilia watu 7 ambao walikutwa na baadhi ya vitu pamoja na bastola 1 na Gobole 1 matching risasi zilizokutwa maeneo ya tukio.

Waliokamatwa wanaongea na kusema kote walikopeleka mali kuviuza. Ni juhudi za kusifiwa za mmoja wa wahanga maana aliamua kulifatilia swala.

Hili mpaka mwisho wake baada ya kuvamiwa na risasi kupigwa ndani kwake. Kwa ushirikiano na wasamaria wema waliotoa info pamoja na Kawe Police wamekamatwa. Kidogo twaweza lala kwa Amani sasa.

Fina Mambo alivamiwa na majambazi wafikao wanane nyumbani kwake na kupora mali na fedha.

Screenshot 2013-03-25 at 06.49.53

Screenshot 2013-03-25 at 06.50.00

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents