Burudani

Baada ya Zendaya kujitoa, Alexandra Shipp achukua nafasi ya kumuigiza Aaliyah kwenye filamu ya maisha yake

Filamu kuhusu maisha ya marehemu Aaliyah inarejea tena. Baada ya Zendaya Coleman kujitoa mwezi uliopita, mrembo mwingine amesaini dili la kumuigiza muimbaji huyo wa R&B kwenye filamu ijayo ya kampuni ya Lifetime.

alexandra-shipp
Alexandra Shipp ataigiza kama Aaliyah kwenye filamu kuhusu maisha yake

Kwa mujibu wa mtandao wa The Hollywood Reporter, msichana mwenye miaka 23, Alexandra Shipp atachukua nafasi hiyo.
Shipp ameigizaji kwenye mchezo wa Nickelodeon, “House of Anubis”na ameonekana kwenye episode za “Switched at Birth,” “Awkward,” na “Ray Donovan.”

Wendy Williams, ambaye atakuwa executive producer, ametangaza jana kwenye akaunti yake ya Facebook.

“Wendy and Wendy Williams Productions are proud to announce that they are joining Debra Martin Chase as executive producers on the Aaliyah Lifetime movie! Production begins later this month with Alexandra Shipp playing Aaliyah.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents