Habari

Baada ya ‘Pombe Yangu’ sasa Madee kuja na ‘Tema Mate Tuwachape’

Ni ukweli ulio wazi kuwa hit single ya ‘Sio Mimi’ au kwa jina lingine ‘Pombe Yangu’ ya Rais wa Manzese Madee kutoka Tip Top Connection ni miongoni mwa nyimbo za bongo fleva ambazo ni lazima uzisikie popote uendapo kama sio Radio zote, basi ni bar, club, kwenye bajaji na sehemu zote za burudani au kwenye TV, na Sasa anakuja na single nyingine ‘Tema Mate Tumchape’

Madee

Kupitia akaunti yake ya Instagram Madee ame-share cover ya single hiyo mpya iliyotengenezwa MJ Records.

Meneja wa Tip Top Connection Hamis Tale aka Bab Tale ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo utatoka rasmi Jumatatu ijayo (September 9).

Hivi karibuni Madee alipozungumza na Bongo5 alifunguka juu ya mafanikio makubwa yaliyoletwa na ‘Sio Mimi’ na kusema mpaka sasa amefanikiwa kuingiza zaidi ya milioni 130 kutokana na show mbalimbali alizopata baada ya kuachia wimbo huo. Madee ni miongoni mwa wasanii ambao wako katika tour ya Serengeti Fiesta 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents