Burudani

Baada ya kushinda Tuzo ya MTV EMA, Rais wa Kenya awaalika Sauti Sol Ikulu kwenye B.Day yake kuwapongeza

Ushindi wa kipengele cha ‘Best African Act’ kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards (EMA) umemshawishi Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kuwaalika Ikulu kundi la Sauti Sol kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (Oct 27) ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza.

Sauti_Sol_and_Uhuru
Sauti Sol wakiwa na Rais Uhuru Kenyatta Ikulu ya Kenya

Kundi hilo lililoanzishwa 2005 liliwashinda Davido, Diamond Platnumz na wasanii wengine wa Afrika.

Kupitia akaunti yao ya Instagram walishare picha na kuandika, “Awesome birthday party!! Happy birthday Mr President @ukenyatta #TeamSautiSol #SautiSol4EMA #BestAfricanAct #BestWorldwideAct #MTVEMA.”

Sauti Sol waeonekana kuwa mabalozi wazuri wa muziki wa Kenya hasa katika tuzo mbalimbali za kimataifa, na kwa sasa wanawania kipengele cha ‘World Wide Act.

Source: Ghafla Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents