Michezo

Baada ya kumtwanga Matumla jr, huyu ni bondia mwingine ambaye Mfaume Mfaume anamtaka ulingoni

Takribani wiki mbili zikiwa zimekatika toka lilipofanyika pambano la masumbwi la round 8 lisilo la ubingwa lililofanyika February 5 mwaka huu katika uwanja wa ndani wa Taifa ambapo bondia Mfaume Mfaume alifanikiwa kumtwanga mpinzani wake Matumla jr kwa knockout katika round ya saba na kumsababishia majeraha ya kichwa.

Baada ya pambano hilo kupita hatimaye mbabe huyo anayechipukia kwa kasi katika mchezo wa ndondi mwenye uzito wa kilo 62 ameibuka na kudai kuwa kwa sasa anamhitaji zaidi bondia Cosmos Cheka wakutane hata bila malipo baada ya pambano lao la awali ambalo Cheka alishinda kwa point.

Bondia Mfaume Mfaume mpaka sasa ameshacheza mapambano 15 na kupoteza mapambano mawili pekee likiwemo la Cheka lililopigwa Diamond Jubilee na lingine akipoteza kwa point nchini Switzerland dhidi ya bondia Gabo Veto.

Zaidi msikilize Mfaume hapo juu.

Na Edward Fabian

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents