Picha

Baada ya kumpiga Ngwair: Mashabiki wamwandama Chidi Benz, aomba msamaha, Ngwair asema, ‘I am strong enough to let it go’

By  | 

Ni ngumu kuamini lakini ni kweli Chidi Benz kampiga mshkaji wake wa siku nyingi na waliyewahi kushirikiana kwenye ngoma, 120, Albert Mangwea.

interview chidi ngwair

Kwa mujibu wa blog ya Dj Fetty hivi ndivyo ilivyotokea:

Rapper Chidi Benz, amempiga Cow Bama a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo (usiku wa kuamkia jana Jumapili). Ugomvi huo ulitokea baada ya Chidi kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.

Baada ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua kumuuliza Chidi (ambae mara nyingi huitana Dogo lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chidi aliendelea kuongea kwa hasira na kusema “ndio nimemzingua kwani yeye nani” na kumbadilikia Ngwea ambae pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye meza aliyokua amekaa na washkaji zake. Haikuishia hapo Chidi amkamfata kwenye meza hiyo na kuanza kumuongelea mbaya Ngwea, na ndipo Ngwea akaamua kushuka chini ya jengo kwa nia ya kuondoka.

Watangazaji wa Clouds FM Adam Mchomvu na Dj Fetty wakiwa na Chidi Benz Ambassador Lounge

Watangazaji wa Clouds FM Adam Mchomvu na Dj Fetty wakiwa na Chidi Benz Ambassador Lounge

Akiwa huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga, ikiwa ni pamoja na kumkata na chupa mkononi,na kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.

Nimeongea na Ngwea ambae anasema haoni chochote kilichomfanya kupigwa na msanii huyo. Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi Oystabay kwa ajili ya kumfungua mashtaka, licha ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho alivyopewa na Benz.

Kutokana na kitendo hicho, mashabiki wamemshambulia Chidi kwa matusi ya nguoni kupitia Twitter na hizi ni miongoni mwa tweets hizo:

@cloudcharles91: @chidibeenz umeniboa tena umeniboa sana kumzingua mwanangu @ngwair kama mziki umekushinda kaa pembeni f*la wewe” umepaniki.

@chidibeenz wanaume rijali atutoboi pua punga ww.. Km unajua pgana, kampge Ney na @diamondplatnumz uko.. achana na @ngwair mtu wa watu ote!

The real yunus: @ngwair no beef…mtu wangu wa nguvu malipo ni duniani waache watoboe pua mwisho wa siku watatoboa maeneo ambayo wakitoboa hata kukaa shida.

“@cloudcharles91: @chidibeenz we ms***e hata kama @ngwair kakuzingua ndo umpige umeniboa sana we boya k*** m*ko”

“Hizo bangi za ukubwani broh,, huoni km ni risk kumpiga mtu na chupa?? 2ngempoteza 2naemuhtaji zaidi yako @ChidiBeenz @ngwair.”

“Umeone eh? I swear bange mbaya sana yani nimekushangaa kwa hili @chidibeenz @ngwair pole ngwair my bro get well soon mwaya.”

Kwa upande wake Chidi Benz alioneshwa kusikitishwa na kitendo cha Ngwair kuretweet matusi yanayomwendea yeye.
‘Siamini kama albert una retweet hii kitu, don’t pretend..hawa. Watu ni watu tuu na watabaki watuu tuuu.na maneno.We unatukana now na unafanya iwe ni kitu, mimi kama unahisi nimekosea mimi Naomba nisamehe kama ulivyowasamehe wengine,” alitweet Chidi.

Alimwambiwa pia Fetty, “kitu nachojua pale ni ofisini kwenu hamtakua mmependa picha ya ugomvi, mimi na ngwea hatuna ubaya naomba tusameheane mnisamehe.”

“Mashabiki msisahau na sisi ni mashabiki wa vitu vingine na tuna maisha mengine, na usijudge maisha ya usiku mimi nikosee au wewe au yeye, “aliongea Chidi.

Lakini Ngwair, ameonesha kutopanic na kutweet vitu vya busara na kwamba ameliacha tukio hilo lipite.
“Am never weak but Strong Enough to Let it Go,” ametweet.

“I don’t know how to fight it’s not my art I rap best.”

“Only You! If you are right then there is no need to get angry, And if you are wrong then you don’t have any right to get angry.”

“Stay away from Anger it hurts.”

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments