Burudani

Baada ya Chris Brown kuchelewa ndege, tuzo za Kora kufanyika leo badala ya jana

707710442_zps0adb652e

Tuzo za Kora zilizotakiwa kufanyika jana mjini Abidjan nchini Ivory Coast zimeahirishwa hadi leo baada ya Chris Brown aliyepangwa kutumbuiza kukosa ndege.

Msemaji wa Kora Ernest Adjovi jana jioni alisema badala yake kila kitu kitafanyika leo.

Waandaaji wa tuzo hizo walidai kuwa Chris Brown alikosa ndege na hivyo show ingefanyika Jumatatu lakini chanzo kimoja kilichopo karibu na tuzo hizo kilisema kuahirishwa kwake kumetokana na matatizo ya waandaaji.

Chris anatarajiwa kuwasili leo kwa ndege binafsi ambapo pamoja na kutumbuiza kwenye show hiyo Chris atakuwa na show ya kusisitiza amani barani Afrika kwenye uwanja mkuu wa mpira wa Abidjan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents