Michezo

Azam TV yamwaga mabilioni kwa TFF

Azam Media Ijumaa hii imefanikiwa kusaini mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa miaka mitano wenye thamani ya shilingi bilioni mbili ambao utakifanya kituo cha Azam TV kuwa na haki ya kurusha mashindano ya ligi ya wanawake na vijana U20.

3493423000000578-3607328-image-a-78_1464115265704

TFF imepanga kuanzisha ligi kuu ya mpira wa miguu kwa wanawake ambayo itaanza mwaka 2016/2017 kwa kushirikisha timu 10 za wanawake huku ligi ya vijana U20 itakayoshirikisha vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Kikao hiko kilihudhuriwa na rais wa TFF, Jamal Malinzi, Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Ltd, Rhys Torrington na Mwenyekiti wa Kamati ya Soka ya Wanawake ya TFF Amina Karuma.

Aidha rais wa TFF alisema, “Tunajua kuna timu nyingi za wanawake hapa jijini Dar, lakini nitoe angalizo tu kwamba hii ligi ni ya Tanzania kwa jumla, hivyo tutaangalia namna ya kupata timu kutoka mikoani na siyo kuegemea Dar es Salaam pekee.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents