Burudani

AY na Shaa waungana na mastaa wengine wa EA kuwa ma-mentor kwenye show mpya ‘Maisha Superstar’ ya Maisha Magic

Ambwene Yessaya na Shaa wamekuwa wakisafiri sana kwenda Kenya miezi ya karibuni, na miongoni mwa vinavyowapeleka huko ni reality show mpya ya kusaka vipaji vya muziki Afrika Mashariki ya kituo cha Televisheni cha Maisha Magic cha DSTV iitwayo Maisha Superstar.

maisha supersta

AY na Shaa wameungana na mastaa wengine wa Afrika mashariki akiwemo Jose Chameleone na Maurice Kirya wa Uganda, Nameless, Erick Wainaina na Rabbit wa Kenya kama ma-mentor kwenye show hiyo.

“Ni kama Tusker Project Fame, lakini haikai hivyo yenyewe inakuwa na Mentors, kwahiyo kila mmoja anakuwa na artist wake anamtengeneza anamwongoza anamwelekeza jinsi ya kufanya, halafu wanakuja wanashindanishwa, mi nina artist wangu, Shaa ana artist wake Nameless ana wakwake Chameleone anae wa kwake hivyo hivyo, sisi ni mentors,” AY ameiambia Bongo5.

‘Maisha Superstar’ itaanza kuonekana rasmi February 9, 2015

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents