Burudani

AY na producer wa ‘Speak With Your Body kusababisha tena?


Kuna dalili kuwa mambo makubwa yako mbioni kutokea tena kati ya producer wa ‘Speak with your body’ wa AY na Lamyia Good.

Riley Urick aliyeproduce ngoma za Sean Kingston,Romeo,Master P,Meek Mill,Tyga, Amerie na pia Engineer kwa Kanye,Akon,Beyonce na Lady Gaga ndiye aliyekuwa nyuma ya mdundo huo ambao pia Romeo alishirikishwa.

Kutokana na mazungumzo kati ya AY, Riley Urick, Hemdee Kiwanuka (promoter wa kimataifa) na rapper Kurtis Blow kupitia Twitter, kitu kikubwa kinaweza kuwa jikoni muda si mrefu.

Hemdee alitweet kwa Riley na Kurtis ambao wapo ziarani barani Ulaya, “I wish I came with you guys. Kill every show so that we go back to Europe with our entire crew!” Ndipo Riley akamjibu,


Naye AY akajibu kwa kuandika, “M ready hommiez, SOON I’l be der.”

Maongezi hayo yakafungwa na Riley na Kurtis walioandika, “
Let’s get it! Lets DO IT!!!

Kurtis Blow Jr ni mtoto wa Kurt Walker aka Kurtis Blow ambaye ni rapper na record producer. Ni rapper wa kwanza kufanikiwa kibiashara na wa kwanza kusaini mkataba wa record label kubwa (Mercury).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents