Promotion

Ay Kupongezwa Na Party Ya Kutwaa Tuzo Ya Channel O Kesho

,

Kadi ya Mwaliko kama inavyojieleza yenyewe.
Msanii Ambweye Yessaya almaarufu kama Ay kesho anatarajiwa kufanyiwa pati maalum kwa ajili ya kumpongeza kwa kutwaa tuzo ya Most Gifterd African East Video Of The Year kwa video ya wimbo “I Don’t Wanna Be Alone” alioshirikiana na wasanii Sauti Sol kutoka Kenya.
Ikumbukwe AY ni official ambasador wa mtandao wa Airtel ambao ndio wadhamini na waandaaji wa party hiyo ya kumpongeza inayotarajiwa kufanyika kuanzia majira ya saa tatu za usiku katika kiota cha burudani Nyumbani Lounge eneo la Namanga Msasani.
AY alitwaa tuzo hiyo wiki mbili zilizopita katika jiji la Johannesburg katika kitongoji cha Soweto katika sherehe ya utoaji na ukabidhi tuzo zilizokuwa zimepewa jina la Channel O Music Video Awards 2012, katika ukumbi wa Kliptown uliopo Walter Sisulu Square.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents