Burudani

AY kuanzisha shamba la mfano kuhamasisha kampeni ya ‘Do Agric’

Msanii mkongwe wa muziki nchini Ambwene Yesayaaka AY, amesema baada ya kumaliza wimbo wa kampeni ya kuhamasisha kilimo anatarajia kuanzisha shamba la mfano ili kuwahamasisha zaidi watu kujihusisha na kilimo.

AY2
Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds FM jana, AY alisema atajaribu kushauriana na One Campaign na kama wakikataa atafanya yeye kama yeye ya bila kumshirikisha mtu.

“Kinachofuata nadhani ni vitendo sasa kwasababu tumeweza kuimba,tumeweza kushoot video na kupromote nyimbo imewafikia wananchi,” alisema rapper huyo. “Lakini la msingi linalotakiwa kufanyika sasa hivi ni sisi wenyewe binafsi pia kuwaonyesha wananchi kuwa tunaweza kufanya ukulima na tuna uhakika tutafanya hivyo,Ukulima bora na wa kisasa na tutawaambia kabisa vijana ambao wanaweza waka invest kwenye kilimo. Kilimo sio cha wazee wala kilimo sio cha watu wa vijijini peke yake,” aliongeza. “Sio kwamba sina mashamba ninayo lakini nataka niwe na shamba ambalo ni la mfano. Ndio ambalo nataka kulianzisha mimi binafsi nina maana kuwa likiwa na mwamvuli wa One Organization, Let’s say kuwa balozi wa kampuni fulani sio lazima wao wakwambie unatakiwa kufanya a b c d, sometimes na wewe unatakiwa uwapatie idea. Kwahiyo na mimi na uhakika hii ndio idea yangu ambayo nitaiendeleza na lazima niwaonyeshe sitaki kuishia kwenye kuimba tu. Nataka nikae nao pia chini kuwashauri na kama walikuwa na hii idea basi tutakuwa sawa na nina uhakika hata kama wasipo kuwa sawa nitafanya binafsi, kwasababu kilimo au ujumbe tunao upeleka sio kwaajili ya One peke yake ni kwaajili ya Afrika nzima, ni ujumbe wa kuongeza chakula Afrika.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents