Burudani

AY azungumzia mafanikio ya video ya Asante pamoja na ujio mpya

Msanii mkongwe wa Hip Hop nchni, Ambwene Yessaya aka AY amezungumzia mafanikio ya video ya ‘Asante’ pamoja na ujio wa kazi zake mpya.

https://www.youtube.com/watch?v=MMbKKWvtnyM

AY ameiambia Bongo5 kuwa amepokea pongezi nyingi kutoka kwa director wa video hiyo baada ya kumweka katika ramani ya muziki wa Afrika Mashariki.

“Mimi kila nikimvumbua mtu na watu wanaenda huko, mpaka sasa hivi hapo juzi nilipigiwa simu na yule director anashukuru kwa jinsi ambavyo nimemuweka katika ile ramani ambayo hata wakenya wenzake walikuwa hawawezi kumuweka katika standard yake,” amesema. “Lakini baada ya mimi watu wanaenda huko kushoot video. Kwahiyo naona ni jinsi gani kumbe ninaweza kuchagua kitu ambacho watu wengi watakiuata. Hata pale nyuma nilipofanya na Ogopa watu na wao wakafuata na kufanya hivyo hivyo. Kwahiyo wimbo bado upo kwenye rotation na kwenye chart mbalimbali. Mwezi ujao nataka niachie mashine nyingine. Mimi ni kama kawaida yangu video na audio, audio ziko sawa zipo kwenye library na siku zinapozidi kwenda ndo tutaendelea kurelease nini kinaendelea kwahiyo watu wakae mkao wa kula.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents