Burudani

AY aliweka ‘appointment ya kukutana na Dr Dre Marekani, wapanga mahali na siku lakini..

Ambwene Yesaya aka AY, hakwenda Marekani kushoot video ya ‘Touch Me’ aliyomshirikisha Sean Kingston na Ms Triniti pekee, alitaka kukutana pia na producer mkongwe, Andre Romelle Young aka Dr Dre ambaye ni role model wake.

10622738_10152458057943379_8729955986986467184_n

“Nilijaribu kumtumia Sean Kingston, lakini ilishindikana,” AY ameliambia gazeti la Daily Nation la Kenya. “Tulikuwa tumeshapanga kabisa sehemu ya kukutana na muda, lakini (Dr Dre) hakuweza kufika sababu alibanwa na mambo mengine,” alisema AY.

“Kinachoridhisha zaidi ni ule ukweli kwamba alifahamu kuwa kulikuwa msanii wa Kiafrika kutoka Tanzania aliyetaka kuonana naye. Hivyo wakati ujao ntajaribu tena.”

Pamoja na kutokutana na Dre, AY alikutana mastaa wengine kama Soldier Boy, mchezaji mieleka wa zamani Hulk Hogan na wengine.

Kwa upande mwingine, AY alidai kuwa hakumlipa chochote Sean Kingston kufanya naye ngoma hiyo.

“Sikumlipa Sean hata senti. Huu ni mradi uliofanyika kwa nia njema na kupitia ukaribu tuliokuwa nao kwa miaka mingi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents