Burudani

AY akutana na Youtube kuzungumza biashara

Baada ya kurejea kutoka Marekani alikoenda kushoot video mbili, Mzee wa Commercial, AY amesema akiwa huko alikutana na wawakilishi wa Youtube waliompa darasa la kuingiza fedha kwenye mtandao huo.

ay

AY amedai kuwa ameshauriwa kujiweka vizuri kwenye mitandao kwakuwa kuna pesa nyingi ambazo hazipaswi kuachwa.

“Kikubwa kwanza nilifanya meeting na Youtube,” AY ameiambia Bongo5. “Kikubwa nilichokiangalia jamaa wana-focus sana kupata pesa kwenye mitandano, kwahiyo nime-discuss na watu wa Youtube. Sasa hivi inabidi tu focus na soko la online tusiliache. Tuendelee kuli-motivate ili watu wazidi kuwa wengi. Sasa hivi linakufanyia urahisi wewe kutokwenda kununua kitu linafanya kila kitu hapo hapo. Pia kuna vitu vikubwa vitakuja baadaye kwa sababu kuna owner wa studio kubwa za Miami tumefanya mazungumzo nao hope tutaenda kufanya kazi Miami na artist wa kule, itakuwa mwakani,” ameongeza.

Katika hatua nyingine AY amesema upo uwezekano mkubwa ndani ya mwaka huu akaachia video moja aliyofanya Marekani.

“Wiki hii nasubiri video ya mimi na Sean Kingston ‘Touch me’ nimeongea nao jamaa jana walikuwa bado wanafuatialia then wanitumie niangalie nione kama kuna tatizo lolote au kama kuna sehemu ya kubadilisha na baada ya hapo itaachiwa.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents