Burudani

Awilo Longomba amwagia sifa Diamond

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo, Awilo Longomba ameshindwa kuzuia hisia zake kwa Diamond Platnumz na kuamua kumwagia sifa kupitia mtandao wa Istagram.

Diamond ambaye Alhamisi hii atatumbuiza kwenye tuzo za shirikisho la soka barani Afrika, CAF zitakazotolewa mjini Abuja, Nigeria, alipost video akiwa katika maandalizi ya show hiyo ndipo Awilo naye akaamua kucomment ya moyoni juu ya mkali huyo wa wimbo ‘Salome’.

Kupitia comment hiyo, Awilo aliandika:

Yesss my brother Diamond the best of the best

Diamond ataanza kuperform katika utoaji wa tuzo za mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2016 maarufu kama CAF Glo Awards ambazo zinafanyika Alhamisi hii Nigeria, na January 14 2016 ataperform katika uwanja wa Stade de l’Amitié Libreville wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 40000 wa kabla ya mchezo wa ufunguzi kati ya mwenyeji Gabon dhidi ya Guinea-Bissau.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents