Burudani

Aunt Ezekiel: Sina ujauzito nimenenepa tu!

Habari zilizozagaa mitaani kupitia mtandao wa Instagram kuwa staa wa filamu za Kibongo Aunt Ezekiel huenda ni mjamzito, zimekanushwa na muigizaji huyo.

Aunt Ezekiel akimlisha keki JB

Alipoulizwa kupitia U Heard ya XXL ya Clouds Fm kama anatarajia kuwa mama, Aunt amesema hana ujauzito wowote isipokuwa anachojua yeye amenenepa tu na kama mimbo ipo basi watu wataona. Baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza kama ni mjamzito kutokana na muonekano wa tumbo lake kwa sasa.

Pia Aunt amekanusha kuwa na uhusiano na dancer wa Diamond aitwaye Moze Iyobo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents