Bongo5 MakalaBurudani

Audio/Uchambuzi: Ngoma 5 mpya za Bongo usizotakiwa kuzikosa kwenye playlist ya Valentine’s Day

Leo ni siku ya wapendanao, Valentine’s Day. Japokuwa siku hii inayoadhimishwa kila February 14, hutumiwa na watu wengi duniani kama siku ya kuonesha upendo kwa wale wanaopenda, kuanzia wapenzi wao, wazazi, ndugu, marafiki na watu wengine muhimu, Valentine’s Day hutumika zaidi kwa watu wenye uhusiano wa kimapenzi kulitia mbolea zaidi penzi lao kwa kuonesha jinsi wanavyopendana na pia kukumbushana jinsi wanavyotegemeana katika furaha yao.

Valentines-Day-2014

Muziki nao umekuwa ukitumika kama chombo muhimu cha kufikisha ujumbe wa mapenzi kwa wapendanao. Kutokana na ukweli huo, tumekuandalia nyimbo tano mpya ambazo unafaa kuzisikiliza kwenye siku hii.

1. AY ft Adela – Asante

Nafasi ya kwanza inashikwa na AY na wimbo wake Asante aliomshirikisha Dela. Kwenye wimbo huu AY anajaribu kutukumbusha kulitilia maanani neno lenye herufi tano kwa Kiswahili lenye umuhimu mkubwa kwenye uhusiano, ASANTE. Ni lini mara ya mwisho umemshukuru mpenzi wako kwa upendo anaokupa? Kwa mwanaume uliyeoa na umepata mtoto ama watoto, fikiria jinsi ambayo aliamua kuubeba ujauzito uliompa, ukamtesa kwa miezi tisa na kisha kujifungua kwa uchungu?

Baada ya kujifungua amekua akimlea mwanao kwa upendo mkubwa, anakosa usingizi kumwangalia mtoto na kumwangalia saa 24 ndani ya siku saba. Lakini pamoja na yote hayo bado ameendelea kukuonesha upendo wa hali juu, amekuvumilia pale unapomkwaza, kama hukuwa mwaminifu umemuomba msamaha na amekusamehe na wala haoneshi dalili zozote za kuwa na donge moyoni, zaidi ya kuendelea kukupenda, kukuheshimu na kukuthamini kwa moyo wake wote na kukupenda penzi tamu. Umewahi kuwaza anapitia mangapi kuendelea kuwa mwanamke mvumilivu na anayekupenda kwa dhati? Mshukuru na mwambie ASANTE leo kwa haya anayokufanyia.

“Valentine’s ni siku ambayo watu wanaoneshana upendo, siku ambayo watu hawastahili kugombana,” anasema AY. “Na pia ni siku ya kuonesha appreciation kwa mtu ambaye unampenda. La msingi kwasababu mmeishi muda wote kutoka Valentine’s iliyoisha mwaka jana mpaka mwaka huu, mmeshapitia mengi, sababu hapo katikati lazima kuna makwaruzano na vitu kama hivyo lakini mwisho wa siku unasema tu Asante. Na niliuandika wimbo huu nikiamini kabisa katika watu kumi,watu kumi wote unawahusu kwakuwa najua kabisa huu wimbo hata kama ni jambazi hata kama mtu ana roho mbaya gani lakini ana mtu ambaye anampenda na anastahili kumwambia Asante.”

Kama utaona huwezi kuisema ASANTE kwa kiwango cha kuvutia, basi AY anakusaidia kwenye Valentine’s Day hii kusema.

2. D-Knob ft Mwasiti – Nishike Mkono

D-Knob anakamata nafasi ya pili kwa wimbo wake uliovunja kwa kishindo ukimya wake wa muda mrefu. Hata hivyo wimbo huo unaodaiwa kurekodiwa tangu mwaka 2011 unazungumzia umuhimu wa wapendanao kuonesha penzi lao waziwazi.

Kama kweli unampenda mpenzi wako, sidhani kama utaona aibu kumtambulisha au kumuonesha hadharani kuwa unampenda. Mnapokuwa mmetoka out kwenda kujituliza sehemu, mshike mkono na muoneshe jinsi unavyompenda na kumthamini. Katika Valentine’s Day nadhani D-Knob ametoa ujumbe uzuri wa kuzingatiwa na wapendanao.

Tayari D-Knob na Mwasiti wameshoot video ya wimbo huu na kampuni ya E-Media na imepangwa kutoka siku ya Valentine’s. Wimbo umetayarishwa na producer Villi.

3. Ben Pol – Unanichora

Nafasi ya tatu inakamatwa na Ben Pol. Unanichora ndio jina la wimbo huu uliotayarishwa na Msweden, Fundi Samwel. Ni wimbo mzuri na bora kabisa katika nyimbo zilizoimbwa mwaka huu na ni imani yangu kuwa utadumu masikio kwa wengi hasa kwakuwa unasikika live mno kwa piano na gitaa za ukweli zinazosikika huku Ben akiendelea kutoa makucha ya namna alivyo mnyama katika sauti.

“Maana yangu kiuandishi ni kwamba kuna mtu nampenda sana na sitaki kumpoteza lakini ni ukweli kwamba kweli ananichora na ni ukweli kwamba anakaa na watu wabaya. Kwahiyo mimi katika kuwaza kwangu, nimewaza mpaka nimeenda beyond lakini mwisho wa siku akiniambia tuachane itaniuma,” anasema Ben.

“Kuna watu pia wanasherehekea Valentine’s kwa migogoro na kutendwa, Valentine’s chungu. Kwahiyo kuna watu ambao Valentine’s chungu na wengi Valentine’s nzuri, wote wana nafasi kwenye jamii.”

4. Vanessa Mdee – Come Over

Come Over ni wimbo wa zamani kidogo ukilinganisha na nyimbo za tatu za juu. Lakini harufu ya upya yake bado haijaanza kupotea. Ni wimbo uliomfikisha mbali zaidi Vanessa kuliko ilivyokuwa Closer. Tayari wimbo huu umefanikiwa kushika chart ya redio kubwa ya Nigeria iitwayo Beat FM.

Come Over ni wimbo unaozungumzia msichana aliyemmiss mpenzi wake ambaye upweke unamkosesha raha,. Msichana huyu anashindwa kujizuia kumwaza mpenzi wake na anatamani atoke kokote aliko aje kuipoza hamu yake ya kumuona.

Ni wimbo mzuri kwa wapendanao wanaoshi mbalimbali na ambao umbali wao ama kazi wanazofanya unawafanya wasionane.

“Come over inaweza ikawa an inspiring song to Valentine’s,” anasema Vanessa. Ni wimbo ambao unazungumzia kujaribu kumpata yule ambaye unampenda au unamadmire au ungependa kuspend time naye au ungependa kumwalika kwenye movie.

Come Over is about to initiate a relationship or a friendship or a partnership or conversation between the loved ones, the people who admire each other want to spend time to each other. Nilipata meseji kutoka kwa shabiki mmoja aliniambia kwamba mke wake alikuwa amemkasirikia akamtumia wimbo wa Come Over kwenye Whatsapp ghafla hasira ikaisha and she came back home.”

4. Linex ft Recho – Ndoa au Harusi

Ndoa au Harusi ni wimbo ulioutungwa maalum kwenye harusi ya Miraj Kikwete na mke wake Alma. NIi wimbo wa zouk unaoelezea jinsi wapenzi hao walivyovumiliana hadi kufika kwenye hatua ya ndoa. Unazungumzia jinsi pale Miraj alipolazimika kujishusha ili tu asimpoteze mpenzi wake kwakuwa anampenda.

Sikiliza hapo chini makala hii kwa mfumo wa sauti ambapo utawasikia AY, Ben Pol na Vanessa Mdee wakiongelea nyimbo zao na Valentine’s Day pamoja na kusikia nyimbo hizi 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents