Burudani

Audio: Mimi Mars adai u-MC unamlipa kuliko kazi zake zote, afunguka ishu ya kubaniwa na Vanessa

Msanii wa muziki, Mimi Mars ambaye pia ni mtangazaji wa TV 1 amefunguka kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu maisha yake ya familia na muziki.

Muimbaji huyo ambaye ana degree mbili, ya sheria na Hospitality Industry ambayo inahusiana na masuala ya Utalii, amekiambia kipengele cha Nyuma ya Pazia Kitaa ndani ya kipindi cha Sasamba cha TBC FM, kuwa kwa sasa kazi ambayo inamwingizia pesa nyingi kwa sasa ni u-MC ambao amekuwa akifanya kwenye matukio mbalimbali.

“Kusema kweli kila nilichosomea kinajitahidi lakini katika vitu vyote ninavyofanya u-MC ndio unanipa pesa nyingi zaidi. Muziki ndio nimeanza kwahiyo siwezi kujua labda baadae lakini kwa sasa kazi hiyo ndio inanipa hela nyingi zaidi.

Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Suga’ amewashukuru wadau mbalimbali wanaompatia support katika muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents