Burudani

Audio: JCB azungumzia jinsi wazo la wimbo wake Drive Slow lilivyokuja na kumshirikisha Profesa Jay

Rapper wa Arusha JCB amesema wimbo wake aliomshirikisha Profesa Jay, Drive Slow alikuwa ameuandika tangu miaka miwili iliyopita.

Proff

Akiongea na kipindi Daladala Beat cha Magic FM leo, JCB amesema ni Profesa Jay ndiye aliyemfanya aurekodi na kuutoa kipindi hiki.

“Hii track nilikuwa nimeifanya zaidi ya miaka miwili iliyopita nikawa nimeiweka tu kwenye kabati langu la mistari,” amesema JCB.

“Sasa juzi brother Profesa Jay alivyokuja Arusha tukaa chini akaja home nikawa ninamsikilizisha ngoma zangu, akasikiliza ngoma za kutosha sana, alivyosikia Drive Slow akasema ‘J stopisha hiyo ngoma, tukastopisha. Kumbe mwezi mmoja uliopita jamaa alikuwa amefiwa na mama yake na ajali tena hiyo hiyo ya barabarani.”

JCB amesema Profesa aliporudi Dar es Salaam alimtumia nauli ili aje Dar kuurekodi wimbo huo.

Msikilize zaidi hapa.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/115448770″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents