Burudani

Audio: Gosby akiuelezea wimbo wake mpya ujao ‘Baby Making Swag’ BMS

Rapper aliye chini ya B’Hits Music Group, Gosby anatarajia kuachia ngoma mpya hivi karibuni iitwayo, BMS (Baby Making Swag). Ngoma hiyo imeyatarishwa na Pancho Latino na kumiksiwa na Hermy B wa B’Hits.

Akiongea na Bongo5, Gosby amesema awali wimbo huo ulikuwa uitwe ‘Ndani’ lakini baada ya kuweka status Facebook kuomba watu wampe ushauri kati ya jina hilo ama BMF, wengi walipendekeza BMF.

“Ni wimbo unaoelezea mwanaume amekutana na mwanamke na kama anamseduce fulani hivi ili waende naye kitandani kwamba jamaa anampiga sound kwamba ‘mimi nikiwa na wewe, I will do this, I will do that so twende ndani’ so wimbo design hiyo’ I will give you this baby making swag,” anasema Gosby.

Gosby amesema BMS ni wimbo tofauti kabisa na nyimbo zingine alizowahi kufanya.

“Nimefanya kitu tofauti kabisa, tunataka tujaribu kuusogeza huu muziki uende sehemu tofauti, hata ukipigwa Europe mtu hawezi kuelewa, yaani uwe universal music sio Bongo Flava tu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents