Burudani

Audio: Dogo D amdiss Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, Mo asema kuna watu wanampotosha

Rapper wa Mwanza mwenye umri mdogo aitwaye Dogo D amemdiss hitmaker wa ‘Basi Nenda’ Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, kwenye ngoma yake, Wamenichokoza.

IMG_9806
Dogo D

Kisa cha kumchana Mo Music ni kutokana na kudai alitaka amshirikishe kwenye wimbo wake aliourekodi kwenye studio za Classic Sounds zilizo chini ya producer Mona Gangster lakini hadi leo amekuwa akimchenga.

“Mwanzoni ulipokwenda, pamoja tulikwenda, kuhit Basi Nenda kufanya ngoma yangu ndio unanipiga kalenda,” anarap Dogo D kwenye wimbo huo ambao ni muendelezo wa wimbo wa Nay wa Mitego, Wamenichokoza. Akiongea kwenye kipengele cha Inbox kwenye kipindi cha Next Chapter cha Radio Free Africa, Dogo amedai kuwa kila akimpigia simu Mo Music aende kuweka kipande chake kwenye wimbo huo amekuwa akimpiga kalenda kwa sababu za kuwa kwenye shows.

Kwa upande wake Mo Music amedai kuwa hajakataa kufanya chorus ya wimbo huo bali ratiba zao zimekuwa zikichengana. Mo anasema yeye na producer wake aitwaye Lollipop wamekuwa na mpango wa kumsaidia rapper huyo kwa kugharamia miradi yake ikiwemo video na hivyo anashangaa kumsikia Dogo akimdiss tena.

“Imani yangu sio yeye ndio maana siwezi kumchukia Dogo. Nahisi alichokiandika it’s not Dogo D, yaani nyuma yake kuna watu wanampotosha, hayupo hivyo namfahamu,” Mo Music ameimbia Inbox. “Kwahiyo wakamjaza sumu kwasababu namfahamu Dogo D, ana love na mimi mpaka inapitiliza, kwahiyo kuna watu wanamtengeneza.”

Sikiliza kipengele hicho hapo chini pamoja na kipande cha wimbo wa Dogo D.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents