BurudaniDiamond Platnumz

Audio: Chidi Benz atoa machozi, akumbushia Diamond alivyohangaika kumuomba collabo na alivyotabiri angekuja kuwa staa

Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa.

928363_549738385155616_595677792_n
Chidi Benz akiongea kwa uchungu Jumanne hii kwenye interview na XXL ya Clouds FM

Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake.

Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya ‘Mpaka Kuche’ aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi.

Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali.

Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri.

“Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa,” alikumbushia Chidi.

Chidi alisema Diamond alianza kueleza shida yake na alikuwa akimsikiliza tu huku kicheko kikitaka kumlipuka kutokana na jinsi Diamond alivyokuwa akiongea haraka haraka. “Nikamsikiliza mimi nacheka ndani lakini simuoneshi, namkazia, namwambia ‘aah huwezi kunichukua’. Lakini in a funny way, tukaondoka siku hiyo hiyo nikatoka mpaka studio tukafika kwa Bob Junior kichumba fulani hivi Magomeni,” alisema Chidi.

“Tumemaliza kurekodi nikamwambia ‘sikiliza nakuambia leo, mimi nawaambiaga watu, nilishamwambia Mwasiti, nilishamwambia, nawaambiaga watu ‘wewe utakuja kuwa staa’. Kwahiyo leo mimi nakumbia, nimekufanyia leo umeniondoa nyumbani leo nakufanyia, wewe utakuja kuwa bonge la staa. Ila nakuomba kitu kimoja, nimekuuliza ‘unakunywa’ umesema haunywi, nimekuuliza ‘unavuta’ umesema hauvuti. Nakuomba mimi kwa maneno yangu, usinilipe, usinipe shilingi yoyote, usinipe kitu chochote, usije kunywa pombe, usije kuvuta, wewe fanya muziki. Halafu hivi leo umenifuata, unaniheshimu, kama unaniamkia hivi, baki hivyo hivyo, kuwa hivyo hivyo kwa kila mtu, wewe utakuja kuwa bonge la staa, utakuja utashinda matuzo. Niliishia hapo nikamfanyia verse, nikaondoka.”

Wimbo ambao Diamond alimshirikisha Chidi Benz unaitwa Nalia na Mengi uliopo kwenye album yake ya kwanza.

Hata hivyo Chidi anasema kuwa hataki watu waseme Diamond anamsaidia kwa sasa ili kulipa fadhila kwakuwa hakumsaidia bali alishiriki tu katika sehemu ndogo ya maisha yake.

“Leo wakati natoka kuna mtu alisema hiyo, nikamwambia ‘Diamond ananisaidia sana mpaka najisikia vibaya hivi, naona sijui atakuwa anaongea huko lakini ananisaidia sana najisikia vibaya’. Lakini nikamwambia ‘mimi sijamsaidia yule, usichanganye kusaidia na kuparticipate katika life yake.”

Kwa upande wake Diamond alidai kuwa sababu ya kujitolea kumsaidia Chidi Benz ni kutokana na jinsi yeye alivyosaidiwa kipindi bado hajatoka na hapendi kuona kipaji cha rapper huyo kinapotea hivi hivi.

“Hapo kati nilikuwa nasikia vitu sio vizuri lakini nikajua kabisa matatizo kama hayo yanakuwa yanatokana na .. unajua mtu anapokuwa hajaachia kazi vitu vingine vinakuwa vinaingia matatizo, vitu kama hivyo. Kwahiyo nikawa nasema nikikutana na Chidi namwambia ‘Kwanini usifanye balaa moja? Mimi nipo ukitaka anytime niambie tu kwasababu kama wewe uliweza kunisaidia kwanini mimi unapokuwa na kitu chake nisikusaidie, wewe niambie tu yaani mimi ntajitahidi nifanye kwa hali na mali tupate ngoma nzuri tu,” alisema Diamond.

Akielezea sababu za kulia wakati anaongea kwenye interview hiyo, Chidi alisema ni machozi ya furaha.

“Naona kwa reality life ambayo it’s true mimi naishi na nimeishi hapo katikati pamoja na maneno yote yaliyotokea ambazo mimi najua true or false sio za kuziongelea sasa lakini the real pain I have in my heart, the true life nimeishi hapo katikati na they way hawa jamii walichokifanya, I am happy man, nashukuru sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents