Burudani

Audio: BASATA yafunguka ishu ya Nay wa Mitego kukamatwa, familia ya Nay yatoa neno

Baada ya rappa Nay wa Mitego kutoa taarifa kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba amekamatwa na taarifa hizo kuthitishwa na jeshi la polisi, Bongo5 imezungumza na familia ya rappa huyo pamoja na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) baada ya taarifa kuzagaa kwamba rappa huyo amekamatwa kutokana na wimbo wake mpya uliovuja mtandaoni.

Akiongea na Bongo5 producer wa rappa huyo, Osam Flexible kwa niaba ya familia amesema wao wamezipata taarifa za kukamatwa kwa Nay wa Mitengo mkoani Morogoro kama watu wengine walivyosikia lakini hawajajua sababu ya kukamatwa kwake.

“Ni kweli Nay amekamatwa hata sisi tumepata hizo taarifa na nimetoka kuongea na mama yake na yeye hajui chochote,lakini mtu ambaye alikuwa naye Morogoro naye nimeongea naye amesema ni kweli na polisi amedai wametumwa wamkamate,”

Aliongeza,”Bado hawajasema chochote kuhusu kukamatwa kwake lakini watu wanadai ni kutokana na wimbo wake uliovuja mtandaoni.,”

Baada ya taarifa hiyo Bongo5 ilimtafuta Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa Godfrey Mngereza ambapo yeye alidai hawajatoa taarifa ili akamatwe msanii huyo huku akidai kwa sasa wanajipanga kuandaa adhabu kwajili ya msanii huyo baada ya kuachia wimbo ambao amedai hauna maadili.

“Kuna kitu kinaitwa principle of natural justiste ina maana hii siyo mara ya kwanza wala siyo mara ya pili kwa Nay ambaye anafanya vitu vya ajabu, kwa hiyo usishangae kusikia amekamatwa kwa sababu watu wanasema mkono wa serikali unaenda mahali popote pale,”

Alisema wao kama BASATA bado wanazungumza na wanasheria kuangalia adhabu ya kumpatia baada ya kukagua wimbo huo na kugundua ni mchafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro kutokana na wimbo wake uitwao ‘Wapo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents