Burudani

AT: Muziki hauna matumaini ya kutoa wasanii wapya

Msanii wa muziki wa mduara, AT amesema kwa jinsi muziki wa Tanzania ulivyo kipindi hiki, hakuna dalili za kutoa wasanii wengine na kuwang’arisha.

at2

AT amedai kuwa hali hiyo imemfanya kushindwa kuachia wimbo mpaka atakapopata njia sahihi za kupenyeza muziki wake.

“Niliweka ahadi nitaachia video, lakini mpaka sasa hivi sijaachia kwa sababu muziki wa bongo sasa hivi hauna matumaini ya kutoa watu wapya,” AT ameiambia Bongo5.

“Kwa sababu muziki wetu umebadilika hauna tofauti na wa wakenya sio rahisi kutoka ma-underground. Kwahiyo mimi nilikuwa natafuta njia pekee ya bila kutumia hela na wananchi wangu wakapata huduma yangu ambayo nitaitoa. Kwahiyo nimeshamaliza na ninafikiria mwezi huu niuache kwanza na mwezi ujao ndo nianze shughuli yangu ya kuwapelekea watu wangu muziki mzuri.”

AT ameongeza kuwa yeye ni miongioni mwa wasanii ambao hawana pesa za kulipa ili muziki wao upigwe kama wasanii wengine.

“Wale watu wa zamani wote wamepotea kwa sababu sisi hatuna hela,” asema. “Ina maana sisi tukitoa hela ina maana watoe mpaka wasanii wa nje. Haiwezekani mimi nitoe hela halafu Davido asitoe hela. Kama ni hivyo bora tujivue watanzania wote kwenye masuala ya michezo na tufanye masuala mengine. Kwanini sisi tulipe na wengine wasilipe? Ni bora tujiondoe kwenye haya masuala na tufanye mambo mengine.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents