Habari

Askofu Pengo ayataka makanisa kutoshindana kumtumikia Mungu

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa wito kwa makanisa kutoshindana kumtumikia Mungu.

Wito huo umetolewa na askofu huyo Jumapili hii wakati akiongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia, Temboni jimboni humo.

“Tusiingiwe na moyo wa kiburi tukajiona bora kuliko waumini wa parokia nyingine, kwa sababu katika muda mfupi mmefanya makubwa. Kuna watu katika jumuiya zetu wakitambua wewe ndio mkuu, hatari ya kujigamba na kujidai ni kubwa kwamba ni kwa nguvu zako unafanya hayo unayofanya, tukumbuke ukuu unatoka kwa Mungu ndio unaodumu lakini wa binadamu ni ukuu wa kupita,” alisema Pengo.

Aidha Askofu Pengo aliwataka waumini wa makanisa kumtanguliza Mungu mbele na hata kama kuna mambo makubwa wanayafanya, wasijigambe kwa kujilinganisha na makanisa mengine ambayo hayajaweza kufikia walipo, bali kumshukuru Mungu daima kuwafikisha walipofika

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents