Habari

Askofu Gwajima kuzuru IPP Media Ijumaa hii

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Ijumaa hii atatembelea IPP media kwaajili ya kuwapa pole wana tasnia ya habari kwa yaliyotokea.

Ijumaa iliyopita kituo cha Clouds kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.

“Kesho 24/03/2017 nitatembelea ofisi za IPP Media ikiwa ni ziara Ya kuwapa pole wanatasnia ya Habari kwa yaliyotokea,” ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram.

Alhamisi hii Askofu huyo ametembelea EFM redio na TVE.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents