Habari

Askofu Gwajima kuzulu EFM Alhamis hii

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa Alhamisi hii atatembelea kituo cha redio cha Efm pamoja na TVE kwaajili ya kuwapa pole wana tasnia ya habari kwa yaliyotokea.

Ijumaa iliyopita kituo cha Clouds kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.

“Kesho Tarehe 23/03/2017 Saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za EFM na TVE ili kuwapa pole wana tasnia ya Habari kwa yaliyotokea.” aliandika mchungaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Askofu huyo leo alitembelea kituo cha Clouds kwaajili ya kutoa pole kwa yaliyotokea.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents