Burudani

Asikuambie mtu, kufanya movie yako mwenyewe ni muziki mzito – Gelly wa Rhymes

Gelly wa Rhymes anatarajia kuachia filamu yake ya kwanza iitwayo Shangazi mwezi June mwaka huu. Kwenye filamu hiyo ya ‘serious comedy’, ameigiza na Asha Boko.

12950300_540531102821322_1951218530_n

Hata hivyo Gelly ambaye kwenye filamu za nyumba alishirikishwa tu, ameiambia Bongo5 kuwa kupitia filamu hiyo amegundua kuwa kufanya movie mwenyewe si kitu cha mzaha.

“Kuna vitu ambavyo nimejifunza, kama bajeti, bajeti lazima ikatike, huwezi kuwa nayo ikaenda kama ulivyoipanga. Mimi ilifika time mpunga wote ukakata ikabidi niitahiji watu wakanisupport,” anasema Gelly.

“Halafu pia kuna wasanii, Asha Boko ni msanii yuko vizuri sana, yuko on time lakini kuna wasanii unaweza ukamuita mtu akachelewa kufika location ambayo mnaambiwa ni muda fulani hadi muda fulani, mara mtu wa kamera naye akazingua, mara umeme umekatika. Mimi nahisi ni kujipanga tu, project yangu nyingine nitajipanga vitu vingi sana kama kuwa labda na jenereta kabisa in case umeme ukikatika, watu kuandaa chakula yaani kila kitu kinakuwa on set mapema,” ameongeza.

Gelly amesema japo siku za usoni anapanga kusambaza video zake mwenyewe, tayari baadhi ya wasambazaji nchini wameonesha nia ya kuisambaza kutokana na ubora wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents