Promotion

Arsenal yatangaza ushirikiano wa kibiashara na Airtel


Klabu ya soka ya Arsenal ya nchini Uingereza, jana imesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na kampuni ya mawasiliano ya simu barani Afrika ya Airtel.
Mkataba huo unaipa fursa Airtel kutumia bidhaa za klabu hiyo kwenye nchi tano za barani Afrika: Nigeria, Zambia, Ghana, Uganda na Rwanda.
Makubaliano hayo yataisaidia klabu hiyo ya kaskazini mwa London kuwafikia mashabiki wake milionu 42 barani Afrika.
Wateja wa Airtel nchini Nigeria, Zambia, Ghana, Uganda na Rwanda wataweza kujishindia tiketi za mechi kushuhudia mechi zao na kupokea habari kuhusu klabu hiyo kwenye simu zao.
Pia makubaliano hayo yataifanya kampuni ya Airtel kuwa kampuni rasmi ya simu kwenye ziara ya mwaka huu ya Arsenal nchini Nigeria.
Arsenal pia itasupport program ya soka ya Airtel Rising Stars, mafunzo ya kila mwaka yanayowapa vijana wa Afrika fursa ya kucheza soka na kushindana kwenye mazingira salama.
Airtel huchangia fedha kwa kila goli linalofungwa kwenye shindano hilo kusaidia elimu ya wachezaji hao kuhakikisha kuwa wale wanaoshiriki hawapati tu mafunzo bora ya mchezo huo bali pia fursa za masomo zaidi ya darasani.

Mkuu wa ushirikiano wa kimataifa wa Arsenal, Vinai Venkatesham alisema: “Nimefurahi kuwakaribisha Airtel kwenye familia ya washirika wa kibiashara. Haya ni makubaliano makubwa ya pili na marefu kutokea barani Afrika na tunaratajia kufanya masuala mengi na Airtel, tukianza na ziara ya Nigeria mwezi August.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents