Michezo

Antonio Conte kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu la Italia, Carlo Tavecchio amempendekeza aliyekuwa kocha wa zamani wa Juventus, Antonio Conte kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia. Kocha huyo amewahi kushinda mataji matatu ya Serie A akiwa na Juventus.

Antonio_Conte-Juve

Conte atachukua nafasi ya Cesare Prandelli, aliyejiuzulu baada ya Italia kutolewa na Uruguay kwenye Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil katika hatua ya makundi na hivyo kuamua kujiunga na Galatasaray.

Mshahara wake unatazamiwa kuwa pauni milioni 2.8 kwa mwaka aliokuwa akilipwa Juventus huku Chama cha FA cha Italia kimeripotiwa kutafuta msaada kutoka kwa wadhamini Puma ili kusaidia kulipa mshahara wa Conte.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents