Burudani

Anne Kansiime, MC Pili pili na Fred Omondi kutoa burudani Jumamosi hii Golden Tulip

Mchekeshaji wa Uganda, Anne Kansiime, Fred Omondi wa Kenya na MC Pili Pili wa Tanzania, wanatarajiwa kutoa burudani siku ya Jumamosi kwa mashabiki wao katika ukumbi wa Golden Tulip.

Anne Kansiime akizungumza na waandishi wa habari
Anne Kansiime akizungumza na waandishi wa habari

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, Anna Kasiime amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi. “Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu. ‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

Mchekeshaji wa Kenya Fred Omondi
Mchekeshaji wa Kenya Fred Omondi

Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku huo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake. Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band. Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.

‘Usiku wa kesho ni maalumu kwa watanzania kufurahia utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert. Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents