Burudani

Angel Mary Kato (BSS): Niliandika ‘No Stress’ baada ya kuumizwa vibaya kimapenzi

Mshiriki wa shindano la Bongo Star Search mwaka 2015, Angel Mary Kato ambaye alifanikiwa kuingia katika Top 5 ya shindano hilo amefunguka sababu ya kuachana na mpenzi wake aliyempelekea kuumia hadi kuandika wimbo wa ‘No Stress’.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, muimbaji huyo amefunguka kwa kusema kuwa mwanzoni alikuwa akimuamini zaidi mpenzi wake huyo lakini alikuja kugundua kuwa alikuwa akidanganywa.

“Nilimpenda sio kwaajili ya chochote, eti mara yupo hivi sijui six figure, sijui nini no I just like a person kama ndivyo. And nilimthamini sana then mwanzoni it was good lakini baadaye kuna action fulani anakuonyesha kama wewe upo by the way, yaani wewe ni kama third party tu.”

“Baadaye ni kaanza kujiuliza maswali nimefanya nini labda imekuaje, later on nikadiscover kwamba nilikuwa kama side chick ambapo sikuwa najua, kumbe he was playing me all the way since mwanzoni hadi mwishoni, kwahiyo nilikuwa najiuliza how come mtu anaweza kukubali kutumia watu wengine in that of way kimapenzi you know something like that,” amesema Angel.

“Iliniuma sana kwamba people are using each other in relationship, sielewi yaani sikuelewa. Labda aliniona ukarimu wangu au upole wangu ndio akaamua anitumie hivyo. So that thing real;y hurt me for the first time, najua kwamba watu wengi it’s not just me, watu wengi wamepitia this experience so what can I do, yes I felt it so many people feel it lakini utafanya nini. Hebu nitengeneze kitu ambacho akisikia next time au mtu akimuumiza hivyo au kama umeshaumizwa hautajisikia kama nilivyokuwa najisikia hautakaa chini na kuanza kulia, hautaanza kujiuliza maswali nini nini! Hamna you will just stand up endelea na maisha yako sema okay fine, no stress acha niendelee na maisha yangu it has happened, however I ‘ll get another good person, basi.” ameongeza.

“Ila obviously hawaruhusu kwamba umetoka halafu unaenda immediately nyingine, no inabidi uchukue time self searching nini nini, jielewe kwanza angalia, tulia halafu ndio uingie katika mahusiano mengine.”

Hata hivyo muimbaji huyo ameongeza kuwa anaamini muda si mrefu video ya wimbo wa ‘No Stress’ itatoka japo kikwazo kikubwa anachokutana nacho kwa sasa ni fedha za kuweza kumsaidia kutengeneza video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents