Michezo

Andy Murray na mkewe wapata mtoto wa kike

Mke wa mchezaji tenisi namba mbili kwa ubora duniani Andy Murray, Kim Sears, amejifungua mtoto wa kike, BBC imebaini. Mtoto wa kwanza wa wanandoa hao inaaminika kuwa alizaliwa Jumapili.

30C87CF500000578-0-image-a-1_1455008540028

Wawili hao Walioana katika mji aliko zaliwa Murray wa Dunblane mwezi Aprili mwaka uliopita.

Murray, alizungumzia kuhusu matarajio yake baada ya kuwa baba katika mashindano ya mwezi uliopita ya Australian Open, alisema kuwa familia yake itakuwa “kipaumbele”. Alisema bayana kwamba angelikatiza mchezo wake wa mwaka na kurejea nyumbani kama mwanaye angelizaliwa mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Alisema: “Mwanangu ni muhimu zaidi kwangu, na mke wangu ni muhimu zaidi kwangu, kuliko mechi ya Tennis . “Ni mabadiliko makubwa kwangu na kwa mke wangu, lakini kwa sasa ndio kipaumbele changu, na tutaona baada ya hilo.
“Sijui hilo litabadili vipi mambo. Bado napenda tenisi.”

Murray alifika fainali katika Australian Open na huku akitokwa machozi alimweleza mkewe: “Nasubiri ndege inayofuata kuelekea nyumbani.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents