Michezo

Amis Tambwe asajiliwa na Yanga baada ya Simba kumtema

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba na kuachwa na klabu hiyo, Amis Tambwe amesema ataidhihirishia timu hiyo ya Msimbazi kwamba kiwango chake bado kiko juu baada ya kusajiliwa na Yanga.

TAMBWEEE
Amis Tambwe akisaini mkataba wa kujiunga na Yanga

“Mimi sina kinyongo ninachotaka ni kuwaonyesha Simba kwamba uwezo wangu wa kucheza bado uko juu,” alisema.

Raia huyo wa Burundi aliahidi kuitumikia vyema Yanga aliyosaini nayo mkataba wa mwaka mmoja. Msimu uliopita Tambwe aliibuka mfungaji bora katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents