Burudani

Talaka ya Amber Rose na Wiz Khalifa: Kila mmoja anamshutumu mwenzie kuchepuka

Ndoa ya Wiz Khalifa na Amber Rose imefika ukingoni. Amber Rose anamshutumu Wiz Khalifa kuwa amekuwa akimsaliti kwa kipindi kirefu na kumtolea sababu zisizo na kichwa wala wa miguu.

1411580687070_Image_galleryImage_LAS_VEGAS_NV_MAY_24_Rappe

Vyanzo vilivyo karibu na Amber, vimeiambia TMZ kuwa tangu kuanza kwa ziara ya Wiz, July mrembo huyo amekuwa akimhisi mume wake kuchepuka. Amber anawaambia marafiki zake kuwa alitaka kuungana na Wiz kwenye ziara hiyo lakini (Wiz) alikataa na kumtaka akae nyumbani kumwangalia mtoto wao.

Anadai kuwa Wiz anataka kumtawala zaidi kwa kusema yeye ndiye anatakiwa kutafuta mkate wa kila siku na Amber akae tu nyumbani.

Naye Wiz anadai kuwa ni Amber ndiye aliyemsaliti na Nick Cannon.

1411578478376_Image_galleryImage_24_AUGUST_2014_LOS_ANGELE

Kupitia talaka hiyo, Amber anataka kuchukua udhibiti wa mtoto wao Sebastian, mwenye umri wa mwaka mmoja lakini atamruhusu Wiz kumtembelea mwanae. TMZ imedai imeziona nyaraka za talaka ambazo zinaonesha kuwa wapenzi hao waliachana Jumatatu hii kwa kile kilichodaiwa tofauti zisizosuluhishika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents