Habari

Aliyekamatwa UK siyo Matonya

Aliyekamatwa UK siyo Matonya
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa kumekuwa na maneno mitaani kwamba mtu mzima Matonya alikamatwa nchini Uingereza na madawa ya kulevya, hayo yote siyo kweli na inasemekana kwamba aliyekamatwa ni mtu anayefanana sana na Matonya.


Mtu mzima Matonya aliibuka ndani ya show ya Tugawane Umaskini
iliyofanyika Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee na
alipoulizwa juu ya maneno hayo alisema: "Unajuwa Mwana hata mimi
nimesikia habari hizo, sijui zimekujaje lakini nilipo ongea na Babu
Tale (Kiongozi wa Tip Top Connection) akaniambia kuna jamaa kakamatwa
amefanana sana na mimi, hilo ndilo ninalojuwa, mwana mimi napiga mziki
siuzi unga" alisema Matonya.

Habari zaidi zinasema wakati tukio hilo linatokea London, Matonya
alikuwa Jijini Arusha akikamua kwenye show ya valentine (tarehe 14
mwezi wa pili) iliyoandaliwa na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents