Burudani

Alikiba ni mkubwa kuliko Davido na Wizkid Lubumbashi,– asema staa wa filamu wa DR Congo

Alikiba ni msanii mkubwa kuliko Davido na Wizkid jijini Lubumbashi, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa mujibu wa staa wa filamu wa nchini humo, Iqbar Mohamed Bagati.

Mohamed2
Iqbar Mohamed Bagati

Lubumbashi ni mji wa pili kwa ukubwa DR Congo baada ya Kinshasa.

Akiongea na Bongo5, Mohamed ambaye yupo nchini alipokuja kutengeneza connection na waigizaji wa Tanzania, amedai kuwa Alikiba anaweza kujaza uwanja wa mpira hata kwa siku tatu mfululizo kwa jinsi anavyokubalika huko.

13285368_993211567429703_1478961834_n

Amesema kuwa staa huyo wa ‘Aje’ ni kipenzi cha watu wengi jijini humo hususan wanawake.

“Alikiba anamshinda Davido, Wizkid, labda tunaweza kumlinganisha na akina P-Square huko Lubumbashi,” amesema Mohamed. Davido alishawahi kutumbuiza mjini humo kwa takriban mara nne na P-Square karibu mara mbili.

“Alikiba ni maarufu sana Lubumbashi.”

Mohamed amesema kama Alikiba akiamua kwenda huko Lubumbashi atashangaa mapokezi atakayoyapata.

Lukumbashi ni jiji lililopo kwenye jimbo la Katanga na ni nyumbani kwa klabu ya TP Mazembe. Watu wengi wa jimbo hilo huongea Kiswahili vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents