Burudani

AliKiba na Mr Blue waungana kumrudisha Abby Skills

Msanii ambaye alifanya vizuri kipindi cha nyuma na nyimbo ‘Maria’ na ‘Mimi na Wewe’ Abby Skills anajipanga kurudi upya katika game la muziki na wimbo ‘Averina’ akiwa na Ali Kiba.
alikiba

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa AliKiba na Mr Blue ndiyo watu ambao wanamsimia kwa sasa ili kumrudisha upya kwenye chati.

“AliKiba na Mr Blue walikaa chini na kuamua kunisaidia kunirudisha kwenye game,” alisema Abby. “Waliniambia tumeona una kipaji kizuri, una melody ngoja tushirikiane ili kukupeleke sehemu fulani,”

Aliongeza, “Hata hii project yangu mpya na AliKiba ‘Averina’ wao ndio wanasimamia kila kitu, kwa hiyo kuna mambo mazuri yanakuja hivi karibuni,”

Muimbaji huyo amesema kazi yake mpya aliyomshirikisha AliKiba itatoka hivi karibuni kwa kuwa tayari ameshashoot na video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents