Burudani

Alikiba azungumzia uwezekano wa kufanya wimbo na Diamond Platnumz

Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia.

Alikiba - Mwana Cover Done Mwana & Kimasomaso
Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko.

“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho kitu kipo. Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” alisema AliKiba.

Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents