Burudani

Alikiba azunguka kwenye daladala Dar kukutana na mashabiki wake (Picha)

Mshindi wa tuzo tano za KTMA 2015, Alikiba amewapa mashabiki wake nafasi ya kuonana naye baada ya kuamua kutumia usafiri wa daladala kuzunguka jijini la Dar es Salaam.

Ali Kiba akishuka kwenye basi la Mbagala, Kariakoo
Alikiba akishuka kwenye basi la Mbagala

Muimbaji huyo wa Chekecha alianza safari yake kwa kupanda daladala ya Kariakoo/Mbagala na kutangaza kwa abiria nia yake ya kupanda daladala nao ikiwa ni pamoja na kuwalipia nauli.

Akizungumza na mashabiki kwenye daladala hizo, Alikiba alisema ameamua kupanda daladala kwa kuamini ataweza kukutana na mashabiki wake ambao hawawezi kumuona na kumpa dukuduku zao juu ya muziki anaofanya.

Ali Kiba akiwa ndani ya basi la abiria
Alikiba akiwa ndani ya basi la abiria

“Nimepanda ndani ya daladala pamoja nanyi kutokana na mapenzi mnayonionyesha katika kazi zangu,” Alikiba aliwaambia abiria wa daladala aliyokuwa amepanda.

“Nisingeweza kuwakusanya pamoja watu wote ila nimeona kwa njia hii ninaweza kuonana na baadhi ya mashabiki wa muziki wangu ambao hawana uwezo wa kuonana na mimi. Lakini kubwa zaidi ni kuwashukuru na kunichagua kuwa msanii ninayependwa. Nimepewa tuzo nyingi kwaajili yenu sina cha kuwalipa zaidi ya shukrani tu. Pia kila mmoja ndani ya daladala nimemlipia nauli, kwahiyo kama kuna yoyote mwenye maoni au ushauri au swala anaweza uliza,” aliongeza staa huyo.

Baada ya kauli hiyo mashabiki mbalimbali walitoa shukrani zao, huku shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Khamis akimtaka Alikiba kuzungumzia ugomvi wake na Diamond pamoja na uwezekano wa kufanya kolabo.

“Sina ugomvi na mtu yoyote, mambo ya kolabo yanawezekana ila ni masuala kiuongozi zaidi,” alijibu Kiba na shabiki huyo kuonekana kuridhika na jibu.

Ali Kiba akipiga stori na abiria
Alikiba akipiga story na abiria

Ali Kiba akishuka katika kituo cha Mtongani
Alikiba akishuka katika kituo cha Mtongani

Ali Kiba akishuka kwenye daladala ya Tememe
Alikiba akishuka kwenye daladala ya Temeke

Ali Kiba akiwa katika kituo cha basi Msimbazi Center
Alikiba akiwa katika kituo cha basi cha Msimbazi Center

Ali Kiba akiwa pamoja na abiria ndani ya daladala ya Temeke/Kariakoo
Alikiba akiwa pamoja na abiria ndani ya daladala ya Temeke/Kariakoo

IMG_1063

IMG_1064

IMG_1070

IMG_1072

IMG_1074

IMG_1075

IMG_1081

IMG_1085

IMG_1096

IMG_1099

IMG_1100

IMG_1107

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents