Burudani

Alikiba asema hana chuki na Diamond, ampongeza lakini…’sifikirii kuongea naye’

Wiki Ijayo Alikiba atakuwa mgeni katika kipindi cha runinga cha The Sporah show. Katika promo ya mahojiano yake na Sporah inayoendelea kurushwa kupitia Clouds TV, Alikiba amemzungumzia Diamond Platnumz ambaye huwa inasemekana wana-beef.

AnD

katika promo hiyo Sporah amemuuliza Alikiba kama Diamond ndiye amechukua nafasi yake kwenye muziki kwa kipindi alichokaa kimya, na majibu yake yanaongeza hamu ya kutokosa kukiangalia kipindi hicho.

Alikiba amejibu kuwa Diamond hajachukua nafasi yake, na kusindikiza jibu lake na mfano wa (nafasi yake) ni sawa na kiti kilichopata vumbi (kwa kutokaliwa siku nyingi) hivyo muda wowote akiamua kurudi anaweza kuamua kukifuta na kukikalia tena. Pia aliongeza kuwa Diamond amekaa kwenye kiti tofauti na yeye, lakini ni yuko ‘back seat’.

Kupitia 255 ya kipindi cha XXL pia leo Alikiba aliulizwa swali kuhusu yukoje sasa hivi na Diamond , haya ndio majibu ya hit maker wa ‘Cinderella’.

“Mimi niko okay sana sema sifikirii kuongea naye tu basi lakini niko very okay yaani. Yaani sijawahi kufikiria si unajua kuwa na mtu okay ni kuzungumza na kuwa karibu unajua hivyo vitu, yaani sijawahi kufikiria hata hivyo. Mi niko okay na sina chuki na sana sana nampongeza lakini sina chuki, simaind yaani niko veeery okay”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents