Burudani

Alikiba adai haufahamu wimbo uitwao ‘Rosa’ uliotoka wiki hii- ‘sijatoa wimbo so far na sijui nani ameimba na sijawahi hata kuisikia’ (Audio)

Sina shaka kama wewe ni shabiki wa Alikiba hukujiuliza mara mbili kuupakua wimbo wa ‘Rosa’ ambao umesambaa wiki hii katika mitandao kama comeback ya star huyo aliyekaa kimya kwa muda mrefu. Lakini cha kushangaza ni kuwa Alikiba mwenyewe hautambui wimbo huo sababu hauko kwenye orodha ya nyimbo alizowahi kurekodi na wala hafahamu mtu aliyeuimba.

Alikiba2

Alikiba amesema amepigiwa simu na vituo vya redio vikimuuliza kuhusu wimbo wake mpya walioupata uitwao ‘Rosa’ lakini hana taarifa nao.

“Nyimbo zipo lakini sija release nyimbo…sijatoa nyimbo so far na sijui nani ameimba na sijawahi hata kuisikia” Alisema Alikiba alipozungumza na mtangazaji Renatus Kiluvya kupitia New Chapter ya Radio Free Africa.

“Sijawahi kuisikia na sitaki kutoa comment yoyote kwasababu navyojijua mimi first of all najikubali sana, la pili watu wananiambia niko unique afu surprise watu wananiambia nimetoa nyimbo sijui tumesikia nyimbo inaitwa Rosa yaani hiyo sijaelewa bado.” Alisema hit maker wa Cinderella.

Aliongeza kuwa kuna uwezekano kuwa kuna watu wamefanya makusudi kufake wimbo huo uonekane ni wake kutokana na ukimya wake, au wamefanya sayansi sauti isikike kama yake, au huyo aliyeimba ni role model wake ndio sababu kaamua kufanya hivyo.

“Wameona nimekaa kimya sana wakaona ngoja watoe nyimbo na wakatumia jina la Alikiba, it doesn’t make sense kama unatoa nyimbo unategemea kutoka kwa jina la mtu flani, I think ni trick moja ambayo imefanywa sielewi na nani lakini I don’t know if in a good way or bad way.”

Pia Ali K alizungumzia ujio wake mpya,
“Ujio wangu uko very soon, sasa hivi wakae tayari fans wangu na kilichonifanya nikae kimya kingi watajua ni kitu gani na watani understand kabisa maana ya kukaa kimya.

Msikilize hapa
[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/141667595″ params=”auto_play=false&hide_related=false&visual=true” width=”100%” height=”450″ iframe=”true” /]

Huu ndio ‘Rosa’ wimbo ambao Alikiba amedai haujui

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents