Burudani

Alicios Theluji, Khaligraph na Christian Bella ndani ya ngoma moja

Muimbaji wa Kenya, Alicios Theluji amefunguka kuhusu wimbo wake unaofuata baada ya ‘Anita’ ambao amemshirikisha rapper Khaligraph Jones wa Kenya na Christian Bella.

Alicios ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo anatarajia kuuachia kabla Valentine’s Day unaitwa ‘Ya Nini’ huku video ya wimbo huo akiwa ameshoot Hanscana.

“I was in studio with Khaligraph Jones who is also featured on Christian Bella’s next single. Their video was shot in Nairobi by Hanscana and I made a special appearance in it. It’s Called Ya Nini,” amesema Alicios.

Hata hivyo picha zao za Instagram zinaonesha kuwa Alicios na Khaligraph walikuwa na session tofauti studio na hivyo kuna dalili za kuwepo nyimbo mbili tofauti zinazowahusisha wasanii hawa.

Wakati huo huo muimbaji huyo ameongeza kuwa wiki hii anatarajia kusaini mkataba na lebo mpyaa ambayo atakuwa anfanya nayo kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents