Burudani

Alichokisema Mwana FA baada ya kile alichokiona kwenye Fiesta Dar kuhusu wasanii wa Bongo

Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ni miongoni mwa wasanii waliopata nafasi ya kupanda jukwaa moja na rapper T.I kutoka Marekani, usiku wa Jumamosi October 18 pale viwanja vya Leaders Club jijini Dar katika tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2014.

FA fiesta

Licha ya kufanya show kali lakini pia Binamu alikuwa ni mtazamaji wa show za wasanii wengine wa Bongo na wale kutoka Nigeria, Kenya pamoja na mkali Clifford Joseph Harris a.k.a T.I.

Hiki ndicho alikiandika FA Instagram siku iliyofata baada ya show ya Fiesta:

“Imani yangu imepata nguvu sana jana, kuwa wabongo wanapenda mno wasanii wao(na mziki wao)..sana,sana…luv za kupitiliza..fundisho tu kuwa hakuna sababu ya kuendelea kubabaikia mziki wa nje(HASA WA KIPOPO)..kwy market hii watu wetu wakipewa nguvu tu wanakinukisha na wanadeliver,hakuna cha wapopo wala ‘wanyamwezi’..tia mkwanja mrefu watu wetu,hakikisha mzunguko wa hela unabaki bongo,tutabeba mziki na uchumi wetu kwa wakati mmoja,ndege kibao jiwe moja.. noma sana jana…noma sana…”

Kauli hiyo ya FA imekuja miezi saba toka atweet: “katika habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa Nigeria..”. Ingia Hapa

fa

Na katika mahojiano na 255 ya XXL alisema:

“Mimi nikiskiliza muziki wa Nigeria hata nikisikiliza ufundi wao jinsi wanavyoimba sioni kama jamaa wanakuwa mafundi hivyo…naamini tuna watu wengi ambao wanaimba vizuri zaidi yao hapa lakini kwasababu watu wanafanya double standards wanauangalia muziki wa Nigeria kivingine na muziki wa kibongo kivingine inakuwa shida…”

Na mwisho alitoa ushauri:

“Ifike mahali tussupport muziki wetu tussupport watu wetu tuone kama tunaweza kupiga hatua”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents