Burudani

Ali Kiba:Nawasaidia wasanii wachanga kutokana na mateso ambayo nimepata

Msanii wa muziki, Ali Kiba amefunguka kwa kusema kuwa anapenda kufanya kollabo na wasanii wachanga ili kuwasaidia kimuziki kwa sababu yeye mwenyewe alipata shida sana kutoka kimuziki.
Ali Kiba

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds Fm, Ali kiba alisema wakati anataka kutoka kimuziki alitamani kutafuta wasanii wakubwa wa kufanyanao kollabo lakini alishindwa.

“Napenda kuwasaidia kutokana na mimi mwenyewe nilipata tabu sana, nilitamani kufanya ngoma na mastaa, lakini kwa bahati nzuri haikutokea, Dully aliweza kufanya nyimbo na mimi kwa mapenzi yake, alinisikia kwa sababu tulikuwa tunakaa opposite, aliweza kusikia bets akaingia moja kwa moja mpaka ndani ,nadhani unamjua Dully mambo yake ya utundu, akaniambia wewe kumbe ni msanii, nikamwambia yeah mimi naimba, akaniambia sawa basi, umefanya wapi?, niikamwambia, kwaiyo akajua mimi nishaendaga mpaka studio, alikuja pale akaamini na mimi nikaimba nilifuraisha sana kwakweli, akasema twende tukafanye , akajaza mafuta gari yake ,yeye mwenyewe kwa pesa yake, sikufichi nasumbuliwa sana, nasumbuliwa sana kwa kollabo , mpaka nikisema hivi anaona kama hawanielewi , lakini mimi nishajua umuhimu wangu ni kuwasaidia , kwaiyo nawasaidia wasanii wachanga kutokana na mateso ambayo nimepata , kwaiyo napenda kuwatoa kama unavyowaona akina Ommy Dimpoz na wengine wengi” Alisema Ali Kiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents