Burudani

Ali Kiba, Saida Karoli na Asley kesho kuibuka kidedea kwenye KORA?

saida nn

Kesho Jumapili ndio siku zitakapotolewa tuzo za thamani za KORA huko nchini Ivory Coast.Wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Ali Kiba, (Dogo) Aslay na Saida Karoli.

Ali Kiba alitajwa kuwania kipengele cha Best Male East Africa kwa wimbo wake Single Boy aliomshirikisha Lady Jaydee ambapo anachuana na Jimmie Gait Feat Dk – Furi Furi Dance, Kenya,Kidum Feat Sana – Mulika Mwizi, Burundi, Redsan – Ila Wewe, Kenya, Chris D – Aisha, Burundi na Mulatu Astatke – Ethiopie, Ethiopia.

Aslay alitajwa kwenye kipengele cha Best Male Newcomer na wimbo wake Niwe Nawe akipambana na Floby – Saanida, Burkina Faso, Loyiso – Wrong To You, Afrique Du Sud, Aziz Azion – My Oxygen, Uganda, Davido – Dami Duro, Nigeria, John Chiti – Wapusuku, Zambie.

Naye Saida Karoli anawania kipengele cha Best Female East Africa kwa wimbo wake Sakina ambapo anachuana na Juliana Kanyomozi – I Am Ugandan, Marya – Shiki Simu, Kenya, Helen Berhe – Lebe, Ethiopia, Asther Aweke – Lu Mili, Ethiopia na Ikraan Caraale – Gaarsiiya, Somalia.

Kwa Tanzania tuzo hizo zitaoneshwa moja kwa moja kupitia Capital Television kuanzia saa tano na nusu usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents