Habari

Album ya Wizkid yapeta kwenye chart ya iTunes duniani lakini mashabiki waiponda

Starboy Wizkid aliamua kufanya kile alichokifanya Beyoncé kwa kuzindua album yake kimya kimya kwenye mtandao wa iTunes.

Wizkid-pic

Hiyo ni baada ya kutweet awali kuwa album yake ya pili ingeingia sokoni leo, 23 September, kisha bila kutoa taarifa akaitoa tarehe 17 September kwenye kwenye iTunes. Hiyo iliwafanya mashabiki wengi kukimbia kwenda kuinunua.

Album hiyo iitwayo ‘Ayo’ au Joy kwa sasa imekamata nafasi ya kwanza kwenye World Music Chart na ipo kwenye album 100 zinazofanya vizuri. Lakini pamoja na mafanikio hayo, mashabiki wengi walionunua album hiyo wamesema haina lolote. Baadhi ya watu walionunua album hiyo wametania kuwa wanataka warudishiwe fedha yao.

Ayo ina jumla ya nyimbo 19 ambazo ni pamoja ‘Jaiye jaiye’, ‘On top your matter’, ‘Show you the money’ na ‘One question’ ambazo hazijawapendezesha mashabiki wake waliosubiri album yake mpya kwa miaka mitatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents