Burudani

Album ya Witnesz ‘Khaya Khaya’ iliyokuwa ikiuzwa Norway pekee kwa sh 30,000 sasa imeanza kuuzwa Tanzania

Rapper Witnesz aliwahi kutoa album inayoitwa ‘Khaya Khaya’ ambayo ilikuwa ikiuzwa nchini Norway peke yake kwa kipindi kirefu, kwa Krone 150 (zaidi ya Tsh 30,0000).

Witnes

Witnesz amesema sasa album hiyo imeanza kuuzwa kwa mashabiki wake wa Tanzania na kutoa sababu za kuanza kuiuza Norway peke yake kwa kipindi kirefu.

Kupitia Facebook ameandika:

“Tsup ma pipo mnaweza kudownload my album now inaitwa khaya khaya ina nyimbo kumi, 1. Usinipige chini 2.khaya khaya 3.salva na witness 4.Tuparana 5.Ni wewe 6.Umwe 7.Kichekesho 8.je m’appelle witness 9.Ndizi 10.it doesnt matter nyimbo za kwenye hii album hazijawahi kutoka Tanzania zaidi ya wimbo mmoja tu uliofanyiwa video ambao ni kichekesho na zingine zote ni mpya kwa pande hizi kwa kuwa album hii ilikuwa chini ya usimamizi wa sigbjorn nedland wa norway chini ya kampuni iitwayo nedland kultur na kuuzwa mjini norway tu kwa kipindi kirefu na sasa inapatikana bongo ndani ya mkito.com just search for kibonge mwepec then khaya khaya, pia demo ya album hii ilifanyika mjini norway na final recording yale ilifanyika Tanzania, kwa kuwa tulitaka kuweka midundo ya asili ambayo ilipigwa live na watanzania wenzetu baadhi ni salum kumpeneka, kaka keppy kiombile,bob rudala ,Cbh na pia ilisimamiwa na producers na sound engineers toka norway kwa ushirikiano na Tanzania, akiwemo morten martins,salvador sanchez pamoja na sigbjorn nedland ambapo ukisikiliza the sounds utasikia utofauti mkubwa sana kwa kuwa vifaa vyote ilipigwa live na sababu za kuchelewa kuiachia Tanzanian ni kwa kuwa kule ilikuwa inauzwa kroner 150 kibongo ni elfu 30 but now unaweza kupata kwa unafuu mkubwa ndani ya mkito.com kwa 2500 album mzima hii yote ni kwa upendo wangu kwenu ninawapenda wote! Ninathamini thamani ya michango yenu pia!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents