Burudani

Album mpya ya Rihanna kuingia sokoni hivi karibuni

Mashabiki wa Rihanna watarajie album ya mrembo huyo siku si nyingi zijazo. Hiyo itakuwa ni album yake ya nane.

rihanna-esquire-uk-3

Akiongea na Entertainment Tonight, Rihanna alidai kuwa album hiyo ambayo imepewa jina la utani R8# itaingia sokoni “very soon.” “Hilo ndio tumaini langu,” alisema. “Ninafurahia sana kuhusu muziki mpya niliokuwa nikirekodi, hivyo nina hamu sana kila mtu aweze kuisikia.”

Riri alidai pia kuwa anaweza akaachia surprise ya wimbo aliofanya na Beyoncé.

Rihanna amekuwa akirekodi studio na watu mbalimbali wakiwemo DJ Mustard, Ester Dean, Ty Dolla $ign, na Ne-Yo.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents